Zab. 17:2-10 Swahili Union Version (SUV)

2. Hukumu yangu na itoke kwako,Macho yako na yatazame mambo ya adili.

3. Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku,Umenihakikisha usione neno;Nimenuia kinywa changu kisikose,

4. Mintarafu matendo ya wanadamu;Kwa neno la midomo yakoNimejiepusha na njia za wenye jeuri.

5. Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako,Hatua zangu hazikuondoshwa.

6. Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,Utege sikio lako ulisikie neno langu.

7. Dhihirisha fadhili zako za ajabuWewe uwaokoaye wanaokukimbilia;Kwa mkono wako wa kuumeUwaokoe nao wanaowaondokea.

8. Unilinde kama mboni ya jicho,Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;

9. Wasinione wasio haki wanaonionea,Adui za roho yangu wanaonizunguka.

10. Wameukaza moyo wako,Kwa vinywa vyao hutoa majivuno.

Zab. 17