1. Ee BWANA, usikie haki, ukisikilize kilio changu,Utege sikio lako kwa maombi yangu,Yasiyotoka katika midomo ya hila.
2. Hukumu yangu na itoke kwako,Macho yako na yatazame mambo ya adili.
3. Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku,Umenihakikisha usione neno;Nimenuia kinywa changu kisikose,
4. Mintarafu matendo ya wanadamu;Kwa neno la midomo yakoNimejiepusha na njia za wenye jeuri.
5. Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako,Hatua zangu hazikuondoshwa.
6. Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,Utege sikio lako ulisikie neno langu.