1. Mungu, unihifadhi mimi,Kwa maana nakukimbilia Wewe.
2. Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu;Sina wema ila utokao kwako.
3. Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora,Hao ndio niliopendezwa nao.
4. Huzuni zao zitaongezekaWambadilio Mungu kwa mwingine;Sitazimimina sadaka zao za damu,Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu.
5. BWANA ndiye fungu la posho langu,Na la kikombe changu;Wewe unaishika kura yangu.
6. Kamba zangu zimeniangukia mahali pema,Naam, nimepata urithi mzuri.
7. Nitamhimidi BWANA aliyenipa shauri,Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.
8. Nimemweka BWANA mbele yangu daima,Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.