4. Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake,Huwapamba wenye upole kwa wokovu.
5. Watauwa na waushangilie utukufu,Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
6. Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao,Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.
7. Ili kufanya kisasi juu ya mataifa,Na adhabu juu ya kabila za watu.
8. Wawafunge wafalme wao kwa minyororo,Na wakuu wao kwa pingu za chuma.