Zab. 149:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Haleluya.Mwimbieni BWANA wimbo mpya,Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.

2. Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya,Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.

3. Na walisifu jina lake kwa kucheza,Kwa matari na kinubi wamwimbie.

4. Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake,Huwapamba wenye upole kwa wokovu.

5. Watauwa na waushangilie utukufu,Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.

Zab. 149