1. Haleluya.Msifuni BWANA kutoka mbinguni;Msifuni katika mahali palipo juu.
2. Msifuni, enyi malaika wake wote;Msifuni, majeshi yake yote.
3. Msifuni, jua na mwezi;Msifuni, nyota zote zenye mwanga.
4. Msifuni, enyi mbingu za mbingu,Nanyi maji mlioko juu ya mbingu.