Zab. 147:4-15 Swahili Union Version (SUV)

4. Huihesabu idadi ya nyota,Huzipa zote majina.

5. Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu,Akili zake hazina mpaka.

6. BWANA huwategemeza wenye upole,Huwaangusha chini wenye jeuri.

7. Mwimbieni BWANA kwa kushukuru,Mwimbieni Mungu wetu kwa kinubi.

8. Huzifunika mbingu kwa mawingu,Huitengenezea nchi mvua,Na kuyameesha majani milimani.

9. Humpa mnyama chakula chake,Wana-kunguru waliao.

10. Hapendezwi na nguvu za farasi,Wala hairidhii miguu ya mtu.

11. BWANA huwaridhia wao wamchao,Na kuzitarajia fadhili zake.

12. Msifu BWANA, Ee Yerusalemu;Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.

13. Maana ameyakaza mapingo ya malango yako,Amewabariki wanao ndani yako.

14. Ndiye afanyaye amani mipakani mwako,Akushibishaye kwa unono wa ngano.

15. Huipeleka amri yake juu ya nchi,Neno lake lapiga mbio sana.

Zab. 147