6. Utupe umeme, uwatawanye,Uipige mishale yako, uwafadhaishe.
7. Uinyoshe mikono yako toka juu, uniponye,Unitoe katika maji mengi, katika mkono wa wageni.
8. Vinywa vyao vyasema visivyofaa,Na mkono wao wa kuume ni mkono wa uongo.
9. Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,Kwa kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia.