1. Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu,Anifundishaye mikono yangu vita,Vidole vyangu kupigana.
2. Mhisani wangu na boma langu,Ngome yangu na mwokozi wangu,Ngao yangu niliyemkimbilia,Huwatiisha watu wangu chini yangu.
3. Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjue?Na binadamu hata umwangalie?
4. Binadamu amefanana na ubatili,Siku zake ni kama kivuli kipitacho.
5. BWANA, uziinamishe mbingu zako, ushuke,Uiguse milima nayo itatoka moshi.
6. Utupe umeme, uwatawanye,Uipige mishale yako, uwafadhaishe.