Zab. 143:4-11 Swahili Union Version (SUV)

4. Na roho yangu imezimia ndani yangu,Moyo wangu ndani yangu umesituka.

5. Nimezikumbuka siku za kale,Nimeyatafakari matendo yako yote,Naziwaza kazi za mikono yako.

6. Nakunyoshea mikono yangu;Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame.

7. Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea;Usinifiche uso wako,Nisifanane nao washukao shimoni

8. Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi,Kwa maana nimekutumaini Wewe.Unijulishe njia nitakayoiendea,Kwa maana nakuinulia nafsi yangu.

9. Ee BWANA, uniponye na adui zangu;Nimekukimbilia Wewe, unifiche.

10. Unifundishe kuyatenda mapenzi yako,Kwa maana ndiwe Mungu wangu;Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa,

11. Ee BWANA, unihuishe kwa ajili ya jina lako,Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni;

Zab. 143