1. Ee BWANA, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu,Kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako.
2. Wala usimhukumu mtumishi wako,Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.
3. Maana adui ameifuatia nafsi yangu,Ameutupa chini uzima wangu.Amenikalisha mahali penye giza,Kama watu waliokufa zamani.
4. Na roho yangu imezimia ndani yangu,Moyo wangu ndani yangu umesituka.
5. Nimezikumbuka siku za kale,Nimeyatafakari matendo yako yote,Naziwaza kazi za mikono yako.
6. Nakunyoshea mikono yangu;Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame.