5. Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili;Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani;Kichwa changu kisikatae,Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.
6. Makadhi wao wakiangushwa kando ya genge,Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu.
7. Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi,Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu.
8. Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana,Nimekukimbilia Wewe, usiniache nafsi yangu.
9. Unilinde na mtego walionitegea,Na matanzi yao watendao maovu.