5. Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba;Wametandika wavu kando ya njia;Wameniwekea matanzi.
6. Nimemwambia BWANA, Ndiwe Mungu wangu;Ee BWANA, uisikie sauti ya dua zangu.
7. Ee MUNGU Bwana, nguvu za wokovu wangu,Umenifunika kichwa changu siku ya vita.
8. Ee BWANA, usimpe asiye haki tamaa zake,Usiifanikishe hila yake, wasije wakajiinua.
9. Nao wainuapo vichwa watu wanaonizunguka,Madhara ya midomo yao yawafunike.