1. Ee BWANA, uniokoe na mtu mbaya,Unihifadhi na mtu wa jeuri.
2. Waliowaza mabaya mioyoni mwao,Kila siku huondokesha vita.
3. Wamenoa ndimi zao kama nyoka,Sumu ya fira i chini ya midomo yao.
4. Ee BWANA, unilinde na mikono ya mtu asiye haki;Unihifadhi na mtu wa jeuri;Waliowaza kuzipotosha hatua zangu.
5. Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba;Wametandika wavu kando ya njia;Wameniwekea matanzi.