Zab. 136:8-18 Swahili Union Version (SUV)

8. Jua litawale mchana;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

9. Mwezi na nyota zitawale usiku;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

10. Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

11. Akawatoa Waisraeli katikati yao;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

12. Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

13. Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

14. Akawavusha Israeli katikati yake;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

15. Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

16. Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

17. Yeye aliyewapiga wafalme wakuu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

18. Akawaua wafalme mashuhuri;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zab. 136