4. Yeye peke yake afanya maajabu makuu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
5. Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
6. Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
7. Yeye aliyefanya mianga mikubwa;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
8. Jua litawale mchana;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
9. Mwezi na nyota zitawale usiku;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
10. Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
11. Akawatoa Waisraeli katikati yao;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
12. Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
13. Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.