Zab. 136:18-23 Swahili Union Version (SUV)

18. Akawaua wafalme mashuhuri;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

19. Sihoni, mfalme wa Waamori;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

20. Na Ogu, mfalme wa Bashani;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

21. Akaitoa nchi yao iwe urithi;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

22. Urithi wa Israeli mtumishi wake;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

23. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zab. 136