17. Yeye aliyewapiga wafalme wakuu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
18. Akawaua wafalme mashuhuri;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
19. Sihoni, mfalme wa Waamori;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
20. Na Ogu, mfalme wa Bashani;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
21. Akaitoa nchi yao iwe urithi;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
22. Urithi wa Israeli mtumishi wake;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
23. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
24. Akatuokoa na watesi wetu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
25. Kila chenye mwili akipa chakula chake;Kwa maana fadhili zake ni za milele.