Zab. 136:16-24 Swahili Union Version (SUV)

16. Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

17. Yeye aliyewapiga wafalme wakuu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

18. Akawaua wafalme mashuhuri;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

19. Sihoni, mfalme wa Waamori;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

20. Na Ogu, mfalme wa Bashani;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

21. Akaitoa nchi yao iwe urithi;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

22. Urithi wa Israeli mtumishi wake;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

23. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

24. Akatuokoa na watesi wetu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Zab. 136