1. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2. Mshukuruni Mungu wa miungu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
3. Mshukuruni Bwana wa mabwana;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
4. Yeye peke yake afanya maajabu makuu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
5. Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
6. Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
7. Yeye aliyefanya mianga mikubwa;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
8. Jua litawale mchana;Kwa maana fadhili zake ni za milele.