1. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2. Mshukuruni Mungu wa miungu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
3. Mshukuruni Bwana wa mabwana;Kwa maana fadhili zake ni za milele.
4. Yeye peke yake afanya maajabu makuu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.