8. Aliwapiga wazaliwa wa kwanza wa Misri,Wa wanadamu na wa wanyama.
9. Alipeleka ishara na maajabu kati yako, Ee Misri,Juu ya Farao na watumishi wake wote.
10. Aliwapiga mataifa mengi,Akawaua wafalme wenye nguvu;
11. Sihoni, mfalme wa Waamori,Na Ogu, mfalme wa Bashani,Na falme zote za Kanaani.
12. Akaitoa nchi yao iwe urithi,Urithi wa Israeli watu wake.
13. Ee BWANA, jina lako ni la milele,BWANA, kumbukumbu lako vizazi hata vizazi.
14. Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake,Atawahurumia watumishi wake.
15. Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu,Kazi ya mikono ya wanadamu.