1. Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,Israeli na aseme sasa,
2. Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,Lakini hawakuniweza.
3. Wakulima wamelima mgongoni mwangu,Wamefanya mirefu mifuo yao.
4. BWANA ndiye mwenye haki,Amezikata kamba zao wasio haki.
5. Na waaibishwe, warudishwe nyuma,Wote wanaoichukia Sayuni.