94. Mimi ni wako, uniokoe,Kwa maana nimejifunza mausia yako.
95. Wasio haki wameniotea ili kunipoteza,Nitazitafakari shuhuda zako.
96. Nimeona ukamilifu wote kuwa na mwisho,Bali agizo lako ni pana mno.
97. Sheria yako naipenda mno ajabu,Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.
98. Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu,Kwa maana ninayo sikuzote.
99. Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote,Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.
100. Ninao ufahamu kuliko wazee,Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.
101. Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya,Ili nilitii neno lako.
102. Sikujiepusha na hukumu zako,Maana Wewe mwenyewe umenifundisha.
103. Mausia yako ni matamu sana kwangu,Kupita asali kinywani mwangu.
104. Kwa mausia yako najipatia ufahamu,Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo.
105. Neno lako ni taa ya miguu yangu,Na mwanga wa njia yangu.