Zab. 119:9-18 Swahili Union Version (SUV)

9. Jinsi gani kijana aisafishe njia yake?Kwa kutii, akilifuata neno lako.

10. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta,Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.

11. Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,Nisije nikakutenda dhambi.

12. Ee BWANA, umehimidiwa,Unifundishe amri zako.

13. Kwa midomo yangu nimezisimuliaHukumu zote za kinywa chako.

14. Nimeifurahia njia ya shuhuda zakoKana kwamba ni mali mengi.

15. Nitayatafakari mausia yako,Nami nitaziangalia njia zako.

16. Nitajifurahisha sana kwa amri zako,Sitalisahau neno lako.

17. Umtendee mtumishi wako ukarimu,Nipate kuishi, nami nitalitii neno lako.

18. Unifumbue macho yangu niyatazameMaajabu yatokayo katika sheria yako.

Zab. 119