Zab. 119:86-89 Swahili Union Version (SUV)

86. Maagizo yako yote ni amini,Wananifuatia bure, unisaidie.

87. Walikuwa karibu na kunikomesha katika nchi,Lakini sikuyaacha mausia yako.

88. Unihuishe kwa fadhili zako,Nami nitazishika shuhuda za kinywa chako.

89. Ee BWANA, neno lako lasimamaImara mbinguni hata milele.

Zab. 119