70. Mioyo yao imenenepa kama shahamu,Mimi nimeifurahia sheria yako.
71. Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa,Nipate kujifunza amri zako.
72. Sheria ya kinywa chako ni njema kwangu,Kuliko maelfu ya dhahabu na fedha.
73. Mikono yako ilinifanya ikanitengeneza,Unifahamishe nikajifunze maagizo yako.
74. Wakuchao na wanione na kufurahi,Kwa sababu nimelingojea neno lako.
75. Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki,Ee BWANA, na kwa uaminifu umenitesa.
76. Nakuomba, fadhili zako ziwe faraja kwangu,Sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.
77. Rehema zako zinijie nipate kuishi,Maana sheria yako ni furaha yangu.
78. Wenye kiburi waaibike, maana wamenidhulumu kwa uongo,Mimi nitayatafakari mausia yako.
79. Wakuchao na wanirudie,Nao watazijua shuhuda zako.
80. Moyo wangu na uwe mkamilifu katika amri zako,Nisije mimi nikaaibika.
81. Nafsi yangu imefifia kwa kuutamani wokovu wako,Nimelingojea neno lako.
82. Macho yangu yamefifia kwa kuitazamia ahadi yako,Nisemapo, Lini utakaponifariji?
83. Maana nimekuwa kama kiriba katika moshi,Sikuzisahau amri zako.