56. Hayo ndiyo niliyokuwa nayo,Kwa sababu nimeyashika mausia yako.
57. BWANA ndiye aliye fungu langu,Nimesema kwamba nitayatii maneno yake.
58. Nimekuomba radhi kwa moyo wangu wote,Unifadhili sawasawa na ahadi yako.
59. Nalizitafakari njia zangu,Na miguu yangu nalizielekezea shuhuda zako.
60. Nalifanya haraka wala sikukawia,Kuyatii maagizo yako.
61. Kamba za wasio haki zimenifunga,Sikuisahau sheria yako.
62. Katikati ya usiku nitaamka nikushukuru,Kwa sababu ya hukumu zako za haki.
63. Mimi ni mwenzao watu wote wakuchao,Na wale wayatiio mausia yako.
64. BWANA, dunia imejaa fadhili zako,Unifundishe amri zako.
65. Umemtendea mema mtumishi wako,Ee BWANA, sawasawa na neno lako.
66. Unifundishe akili na maarifa,Maana nimeyaamini maagizo yako.