49. Likumbuke neno ulilomwambia mtumishi wako,Kwa sababu umenitumainisha.
50. Hii ndiyo faraja yangu katika taabu yangu,Ya kwamba ahadi yako imenihuisha.
51. Wenye kiburi wamenidharau mno,Sikujiepusha na sheria zako.
52. Nimezikumbuka hukumu zako za kale,Ee BWANA, nikajifariji.
53. Ghadhabu imenishika kwa sababu ya wasio haki,Waiachao sheria yako.
54. Amri zako zimekuwa nyimbo zangu,Katika nyumba ya ugeni wangu.
55. Wakati wa usiku nimelikumbuka jina lako,Ee BWANA, nikaitii sheria yako.
56. Hayo ndiyo niliyokuwa nayo,Kwa sababu nimeyashika mausia yako.
57. BWANA ndiye aliye fungu langu,Nimesema kwamba nitayatii maneno yake.
58. Nimekuomba radhi kwa moyo wangu wote,Unifadhili sawasawa na ahadi yako.
59. Nalizitafakari njia zangu,Na miguu yangu nalizielekezea shuhuda zako.
60. Nalifanya haraka wala sikukawia,Kuyatii maagizo yako.
61. Kamba za wasio haki zimenifunga,Sikuisahau sheria yako.
62. Katikati ya usiku nitaamka nikushukuru,Kwa sababu ya hukumu zako za haki.