4. Wewe umetuamuru mausia yako,Ili sisi tuyatii sana.
5. Ningependa njia zangu ziwe thabiti,Nizitii amri zako.
6. Ndipo mimi sitaaibika,Nikiyaangalia maagizo yako yote.
7. Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo,Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako
8. Nitazitii amri zako,Usiniache kabisa
9. Jinsi gani kijana aisafishe njia yake?Kwa kutii, akilifuata neno lako.