166. Ee BWANA, nimeungojea wokovu wako,Na maagizo yako nimeyatenda.
167. Nafsi yangu imezishika shuhuda zako,Nami nazipenda mno.
168. Nimeyashika mausia yako na shuhuda zako,Maana njia zangu zote zi mbele zako.
169. Ee BWANA, kilio changu na kikukaribie,Unifahamishe sawasawa na neno lako.
170. Dua yangu na ifike mbele zako,Uniponye sawasawa na ahadi yako.
171. Midomo yangu na itoe sifa,Kwa kuwa unanifundisha mausia yako.
172. Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako,Maana maagizo yako yote ni ya haki.
173. Mkono wako na uwe tayari kunisaidia,Maana nimeyachagua mausia yako.
174. Ee BWANA, nimeutamani wokovu wako,Na sheria yako ndiyo furaha yangu.
175. Nafsi yangu na iishi, ipate kukusifu,Na hukumu zako zinisaidie.