Zab. 119:154-165 Swahili Union Version (SUV)

154. Unitetee na kunikomboa,Unihuishe sawasawa na ahadi yako.

155. Wokovu u mbali na wasio haki,Kwa maana hawajifunzi amri zako.

156. Ee BWANA, rehema zako ni nyingi,Unihuishe sawasawa na hukumu zako.

157. Wanaonifuatia na watesi wangu ni wengi,Lakini sikujiepusha na shuhuda zako.

158. Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa,Kwa sababu hawakulitii neno lako.

159. Uangalie niyapendavyo mausia yako,Ee BWANA, unihuishe sawasawa na fadhili zako.

160. Jumla ya neno lako ni kweli,Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele.

161. Wakuu wameniudhi bure,Ila moyo wangu unayahofia maneno yako.

162. Naifurahia ahadi yako,Kama apataye mateka mengi.

163. Nimeuchukia uongo, umenikirihi,Sheria yako nimeipenda.

164. Mara saba kila siku nakusifu,Kwa sababu ya hukumu za haki yako.

165. Wana amani nyingi waipendao sheria yako,Wala hawana la kuwakwaza.

Zab. 119