139. Juhudi yangu imeniangamiza,Maana watesi wangu wameyasahau maneno yako.
140. Neno lako limesafika sana,Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda.
141. Mimi ni mdogo, nadharauliwa,Lakini siyasahau mausia yako.
142. Haki yako ni haki ya milele,Na sheria yako ni kweli.
143. Taabu na dhiki zimenipata,Maagizo yako ni furaha yangu.
144. Haki ya shuhuda zako ni ya milele,Unifahamishe, nami nitaishi.
145. Nimeita kwa moyo wangu wote; Ee BWANA, uitike;Nitazishika amri zako.
146. Nimekuita Wewe, uniokoe,Nami nitazishika shuhuda zako.
147. Kutangulia mapambazuko naliomba msaada,Naliyangojea maneno yako kwa tumaini.
148. Macho yangu yalitangulia makesha ya usiku,Ili kuitafakari ahadi yako.
149. Uisikie sauti yangu sawasawa na fadhili zako,Ee BWANA, unihuishe sawasawa na hukumu yako.
150. Wanakaribia wanaonifuatia kwa chuki,Wamekwenda mbali na sheria yako.
151. Ee BWANA, Wewe U karibu,Na maagizo yako yote ni kweli.
152. Tokea zamani nimejua kwa shuhuda zako,Ya kuwa umeziweka zikae milele.
153. Uyaangalie mateso yangu, uniokoe,Maana sikuisahau sheria yako.
154. Unitetee na kunikomboa,Unihuishe sawasawa na ahadi yako.
155. Wokovu u mbali na wasio haki,Kwa maana hawajifunzi amri zako.