Zab. 119:136-148 Swahili Union Version (SUV)

136. Macho yangu yachuruzika mito ya maji,Kwa sababu hawaitii sheria yako.

137. Ee BWANA, Wewe ndiwe mwenye haki,Na hukumu zako ni za adili.

138. Umeziagiza shuhuda zako kwa haki,Na kwa uaminifu mwingi.

139. Juhudi yangu imeniangamiza,Maana watesi wangu wameyasahau maneno yako.

140. Neno lako limesafika sana,Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda.

141. Mimi ni mdogo, nadharauliwa,Lakini siyasahau mausia yako.

142. Haki yako ni haki ya milele,Na sheria yako ni kweli.

143. Taabu na dhiki zimenipata,Maagizo yako ni furaha yangu.

144. Haki ya shuhuda zako ni ya milele,Unifahamishe, nami nitaishi.

145. Nimeita kwa moyo wangu wote; Ee BWANA, uitike;Nitazishika amri zako.

146. Nimekuita Wewe, uniokoe,Nami nitazishika shuhuda zako.

147. Kutangulia mapambazuko naliomba msaada,Naliyangojea maneno yako kwa tumaini.

148. Macho yangu yalitangulia makesha ya usiku,Ili kuitafakari ahadi yako.

Zab. 119