122. Uwe mdhamini wa mtumishi wako, apate mema,Wenye kiburi wasinionee.
123. Macho yangu yamefifia kwa kuutamani wokovu wako,Na ahadi ya haki yako.
124. Kama zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako,Na amri zako unifundishe.
125. Mimi ni mtumishi wako, unifahamishe,Nipate kuzijua shuhuda zako.
126. Wakati umewadia BWANA atende kazi;Kwa kuwa wameitangua sheria yako.
127. Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako,Kuliko dhahabu, naam, dhahabu iliyo safi.
128. Maana nayaona mausia yako yote kuwa ya adili,Kila njia ya uongo naichukia.
129. Shuhuda zako ni za ajabu,Ndiyo maana roho yangu imezishika.
130. Kufafanusha maneno yako kwatia nuru,Na kumfahamisha mjinga.
131. Nalifunua kinywa changu nikatweta,Maana naliyatamani maagizo yako.
132. Unigeukie, unirehemu mimi,Kama iwahusuvyo walipendao jina lako.
133. Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako,Uovu usije ukanimiliki.
134. Unikomboe na dhuluma ya mwanadamu,Nipate kuyashika mausia yako.
135. Umwangazie mtumishi wako uso wako,Na kunifundisha amri zako.
136. Macho yangu yachuruzika mito ya maji,Kwa sababu hawaitii sheria yako.
137. Ee BWANA, Wewe ndiwe mwenye haki,Na hukumu zako ni za adili.