Zab. 119:10-24 Swahili Union Version (SUV)

10. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta,Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.

11. Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,Nisije nikakutenda dhambi.

12. Ee BWANA, umehimidiwa,Unifundishe amri zako.

13. Kwa midomo yangu nimezisimuliaHukumu zote za kinywa chako.

14. Nimeifurahia njia ya shuhuda zakoKana kwamba ni mali mengi.

15. Nitayatafakari mausia yako,Nami nitaziangalia njia zako.

16. Nitajifurahisha sana kwa amri zako,Sitalisahau neno lako.

17. Umtendee mtumishi wako ukarimu,Nipate kuishi, nami nitalitii neno lako.

18. Unifumbue macho yangu niyatazameMaajabu yatokayo katika sheria yako.

19. Mimi ni mgeni katika nchi,Usinifiche maagizo yako.

20. Roho yangu imepondeka kwa kutamaniHukumu zako kila wakati.

21. Umewakemea wenye kiburi,Wamelaaniwa waendao mbali na maagizo yako.

22. Uniondolee laumu na dharau,Kwa maana nimezishika shuhuda zako.

23. Wakuu nao waliketi wakaninena,Lakini mtumishi wako atazitafakari amri zako.

24. Shuhuda zako nazo ndizo furaha yangu,Na washauri wangu.

Zab. 119