Zab. 119:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Heri walio kamili njia zao,Waendao katika sheria ya BWANA.

2. Heri wazitiio shuhuda zake,Wamtafutao kwa moyo wote.

3. Naam, hawakutenda ubatili,Wamekwenda katika njia zake.

4. Wewe umetuamuru mausia yako,Ili sisi tuyatii sana.

5. Ningependa njia zangu ziwe thabiti,Nizitii amri zako.

Zab. 119