8. Ni heri kumkimbilia BWANAKuliko kuwatumainia wanadamu.
9. Ni heri kumkimbilia BWANA.Kuliko kuwatumainia wakuu.
10. Mataifa yote walinizunguka;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
11. Walinizunguka, naam, walinizunguka;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
12. Walinizunguka kama nyuki,Walizimika kama moto wa miibani;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
13. Ulinisukuma sana ili nianguke;Lakini BWANA akanisaidia.
14. BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu,Naye amekuwa wokovu wangu.