2. Israeli na aseme sasa,Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
3. Mlango wa Haruni na waseme sasa,Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
4. Wamchao BWANA na waseme sasa,Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
5. Katika shida yangu nalimwita BWANA;BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi.
6. BWANA yuko upande wangu, sitaogopa;Mwanadamu atanitenda nini?
7. BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu,Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
8. Ni heri kumkimbilia BWANAKuliko kuwatumainia wanadamu.
9. Ni heri kumkimbilia BWANA.Kuliko kuwatumainia wakuu.
10. Mataifa yote walinizunguka;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
11. Walinizunguka, naam, walinizunguka;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
12. Walinizunguka kama nyuki,Walizimika kama moto wa miibani;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
13. Ulinisukuma sana ili nianguke;Lakini BWANA akanisaidia.