Zab. 118:18-27 Swahili Union Version (SUV)

18. BWANA ameniadhibu sana,Lakini hakuniacha nife.

19. Nifungulieni malango ya haki,Nitaingia na kumshukuru BWANA.

20. Lango hili ni la BWANA,Wenye haki ndio watakaoliingia.

21. Nitakushukuru kwa maana umenijibu,Nawe umekuwa wokovu wangu.

22. Jiwe walilolikataa waashiLimekuwa jiwe kuu la pembeni.

23. Neno hili limetoka kwa BWANA,Nalo ni ajabu machoni petu.

24. Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA,Tutashangilia na kuifurahia.

25. Ee BWANA, utuokoe, twakusihi;Ee BWANA, utufanikishe, twakusihi.

26. Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA;Tumewabarikia toka nyumbani mwa BWANA.

27. BWANA ndiye aliye Mungu,Naye ndiye aliyetupa nuru.Ifungeni dhabihu kwa kambaPembeni mwa madhabahu.

Zab. 118