Zab. 118:13-18 Swahili Union Version (SUV)

13. Ulinisukuma sana ili nianguke;Lakini BWANA akanisaidia.

14. BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu,Naye amekuwa wokovu wangu.

15. Sauti ya furaha na wokovuImo hemani mwao wenye haki;Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu.

16. Mkono wa kuume wa BWANA umetukuzwa;Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu.

17. Sitakufa bali nitaishi,Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.

18. BWANA ameniadhibu sana,Lakini hakuniacha nife.

Zab. 118