10. Mataifa yote walinizunguka;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
11. Walinizunguka, naam, walinizunguka;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
12. Walinizunguka kama nyuki,Walizimika kama moto wa miibani;Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
13. Ulinisukuma sana ili nianguke;Lakini BWANA akanisaidia.
14. BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu,Naye amekuwa wokovu wangu.
15. Sauti ya furaha na wokovuImo hemani mwao wenye haki;Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu.
16. Mkono wa kuume wa BWANA umetukuzwa;Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu.