Zab. 116:12-18 Swahili Union Version (SUV)

12. Nimrudishie BWANA niniKwa ukarimu wake wote alionitendea?

13. Nitakipokea kikombe cha wokovu;Na kulitangaza jina la BWANA;

14. Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA,Naam, mbele ya watu wake wote.

15. Ina thamani machoni pa BWANAMauti ya wacha Mungu wake.

16. Ee BWANA, hakika mimi ni mtumishi wako,Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako,Umevifungua vifungo vyangu.

17. Nitakutolea dhabihu ya kushukuru;Na kulitangaza jina la BWANA;

18. Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA,Naam, mbele ya watu wake wote.

Zab. 116