1. Haleluya.Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikilizaSauti yangu na dua zangu.
2. Kwa maana amenitegea sikio lake,Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.
3. Kamba za mauti zilinizunguka,Shida za kuzimu zilinipata.Naliona taabu na huzuni;
4. Nikaliitia jina la BWANA.Ee BWANA, nakuomba sana,Uniokoe nafsi yangu.