Zab. 115:9-15 Swahili Union Version (SUV)

9. Enyi Israeli, mtumainini BWANA;Yeye ni msaada wao na ngao yao.

10. Enyi mlango wa Haruni, mtumainini BWANA;Yeye ni msaada wao na ngao yao.

11. Enyi mmchao BWANA, mtumainini BWANA;Yeye ni msaada wao na ngao yao.

12. BWANA ametukumbuka,Naye atatubariki sisi.Ataubariki mlango wa Israeli,Ataubariki mlango wa Haruni,

13. Atawabariki wamchao BWANA,Wadogo kwa wakubwa.

14. BWANA na awaongeze ninyi,Ninyi na watoto wenu.

15. Na mbarikiwe ninyi na BWANA,Aliyezifanya mbingu na nchi.

Zab. 115