Zab. 115:4-12 Swahili Union Version (SUV)

4. Sanamu zao ni fedha na dhahabu,Kazi ya mikono ya wanadamu.

5. Zina vinywa lakini hazisemi,Zina macho lakini hazioni,

6. Zina masikio lakini hazisikii,Zina pua lakini hazisikii harufu,

7. Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi,Wala hazitoi sauti kwa koo zake.

8. Wazifanyao watafanana nazo,Kila mmoja anayezitumainia.

9. Enyi Israeli, mtumainini BWANA;Yeye ni msaada wao na ngao yao.

10. Enyi mlango wa Haruni, mtumainini BWANA;Yeye ni msaada wao na ngao yao.

11. Enyi mmchao BWANA, mtumainini BWANA;Yeye ni msaada wao na ngao yao.

12. BWANA ametukumbuka,Naye atatubariki sisi.Ataubariki mlango wa Israeli,Ataubariki mlango wa Haruni,

Zab. 115