1. Ee BWANA, kutukuza usitutukuze sisi,Bali ulitukuze jina lako,Kwa ajili ya fadhili zako,Kwa ajili ya uaminifu wako.
2. Kwa nini mataifa kusema,Yuko wapi Mungu wao?
3. Lakini Mungu wetu yuko mbinguni,Alitakalo lote amelitenda.
4. Sanamu zao ni fedha na dhahabu,Kazi ya mikono ya wanadamu.