1. Haleluya.Israeli alipotoka Misri,Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
2. Yuda ilikuwa patakatifu pake,Israeli milki yake.
3. Bahari iliona ikakimbia,Yordani ilirudishwa nyuma.
4. Milima iliruka kama kondoo waume,Vilima kama wana-kondoo.
5. Ee bahari, una nini, ukimbie?Yordani, urudi nyuma?