1. Haleluya.Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote,Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
2. Matendo ya BWANA ni makuu,Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.
3. Kazi yake ni heshima na adhama,Na haki yake yakaa milele.
4. Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu;BWANA ni mwenye fadhili na rehema.
5. Amewapa wamchao chakula;Atalikumbuka agano lake milele.
6. Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake,Kwa kuwapa urithi wa mataifa.
7. Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu,Maagizo yake yote ni amini,