Zab. 110:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Neno la BWANA kwa Bwana wangu,Uketi mkono wangu wa kuume,Hata niwafanyapo adui zakoKuwa chini ya miguu yako.

2. BWANA atainyosha toka SayuniFimbo ya nguvu zako.Uwe na enzi kati ya adui zako;

3. Watu wako wanajitoa kwa hiari,Siku ya uwezo wako;Kwa uzuri wa utakatifu,Tokea tumbo la asubuhi,Unao umande wa ujana wako.

Zab. 110